Alhamisi 8 Oktoba 2026 - 16:00
Wawakilishi wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi Iran, Wamtembelea Ayatullah al-Udhma Nuri Hamadani Hospitalini + Picha

Hawza/ Ujumbe uliotumwa na Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, alasiri ya jana umemtembelea Ayatullah Nuri Hamadani katika hospitali.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Rahimiyan, Muhammadi Araqi, Muhammadiyan na Haj Ali Akbari, alasiri ya jana walifika katika moja ya hospitali za Tehran, ambapo walifikisha salamu za Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa Ayatullah Nuri Hamadani, miongoni mwa Maraji‘ Wakuu wa Taqlidi, na kupata taarifa kuhusu mwenendo wa hivi karibuni wa matibabu na mchakato wa maendeleo ya hali yake.

Wawakilishi hao wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu pia walimtakia Ayatullah Nuri Hamadani afya njema na kupona haraka iwezekanavyo, huku wakieleza matumaini kwamba Hawza hivi karibuni zitaweza tena kunufaika na fadhila na elimu ya Marji‘ huyu mkubwa.

Wawakilishi wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi Iran, Wamtembelea Ayatullah al-Udhma Nuri Hamadani Hospitalini + Picha

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha